Kikisi (Tanzania)

Kikisi ni lugha ya Kibantu nchini Tanzania inayozungumzwa na Wakisi. Isichanganywe na Kikisi-Kaskazini nchini Guinea wala na Kikisi-Kusini nchini Liberia; tena ni tofauti na Kikisii nchini Kenya. Mwaka wa 2001 idadi ya wasemaji ya Kikisi imehesabiwa kuwa watu 10,200. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie, lugha ya Kikisi iko katika kundi la G60.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search